Not for
Reproduction
www.snapper.com
10
!
ONYO:
Mashine hii yenye nguvu ya kukata inaweza kukata mikono na miguu na inaweza kurusha vitu
vinavyoweza kusababisha majeraha na uharibifu! Kutouata maelekezo yafuatayo ya USALAMA kunaweza
kusababisha majeraha mabaya au kifo kwa mwendeshaji au watu wengine. Lazima mwenye mashine
aelewe maelekezo haya na anafaa kuruhusu tu mtu anayeelewa maelekezo haya kuendesha mashine.
Lazima kila mtu anayeendesha mashine hii awe na akili na mwili timamu na hafai kuwa ametumia dawa
zozote, yanayoweza kupunguza kuona, ujuzi au uamuzi.
Linda Watoto
Ajali za kuhuzunisha zinaweza kutokea ikiwa mwendeshaji
hatahadhari kuwepo kwa watoto. Mara nyingi watoto huvutiwa
na kifaa hicho na shughuli ya ukataji nyasi. Watoto ambao
wamewahi kubebwa na kifaa hapo awali huenda wakatokea kwa
ghafla katika eneo la kukata nyasi kwa kutaka kubebwa tena na
wagongwe au kusukumwa na mashine hiyo. Kamwe usidhanie
kwamba watoto watabakia pale ulipowaona mara ya mwisho.
1. WAWEKE watoto mbali na eneo la kukata nyasi na chini ya
uangalizi mkubwa wa mtu mzima anayewajibika ambaye sio
mwendeshaji.
2. USIWARUHUSU watoto katika uwanja wakati mashine
inaendeshwa (hata kama ubapa UMEZIMWA).
3. USIWARUHUSU watoto au watu wengine kupanda juu ya
mashine, viambatisho au kifaa kinachokokotwa (hata kama
ubapa UMEZIMWA). Wanaweza kuanguka na kujeruhiwa
vibaya.
4. USIWARUHUSU watoto wadogo kuendesha mashine.
5. WARUHUSU tu watu wazima & vijana wenye kuwajibika na
wenye uamuzi mzuri waendeshe mashine chini ya uangalizi
wa mtu mzima.
6. USIENDESHE bapa za kukata ukirudi nyuma. SIMAMISHA
BAPA ZA KUKATA. ANGALIA na UONE nyuma na chini
ukitafuta watoto, wanyama kipenzi na uwezekano wa hatari
kabla na wakati unarudi nyuma.
7. KUWA MWANGALIFU ZAIDI unapokaribia kona usizoweza
kuona upande huo mwingine, vichaka, miti, au vitu vingine
ambavyo vinaweza kukuzuia kuona.
Kinga dhidi ya Kupinduka
Miteremko ni chanzo kikubwa kinachohusika na kupoteza
udhibiti na ajali za kupinduka, ambazo zinaweza kusababisha
jeraha kali au kifo. Uendeshaji katika miteremko yote unahitaji
TAHADHARI zaidi. Ikiwa huweza kurudi nyuma kwenye
mteremko au unahisi ugumu katika mteremko huo, USIUKATE
NYASI. Kuwa makinifu zaidi na vinasa nyasi na viambatisho
vingine; hivi huathiri udhibiti na uthabiti wa mashine.
1. USIENDESHE mashine kwenye miteremko inayozidi digrii 10
(kiwango cha 18%).
2. ZIMA bapa zinazopanda mlima. Nenda pole pole na uepuke
kona za ghafla au kona kali.
3. USIENDESHE mashine mbele na nyuma karibu na
mteremko. Endesha juu na chini. Fanya mazoezi kwenye
mteremko ukiwa umezima bapa.
4. EPUKA kuwasha, kusimama, au kugeuka katika mteremko.
Ikiwa mashine itawacha kupanda mlima au magurudumu
yaanze kuteleza, ZIMA bapa na urudi nyuma pole pole hadi
chini ya mteremko.
5. KUWA MWANGALIFU kwa mashimo na hatari zingine
zisizoonekana. Nyasi ndefu zinaweza kuficha vigingi. Epuka
mitaro, mahali penye maji ya mafuriko, kalvati, ua na vitu
vilivyochomoka.
6. WEKA UMBALI SALAMA (angalau pana mbili za mashine
ya kukatia nyasi) mbali na ukingo wa mitaro na miteremko
ingine. Mashine inaweza kubiringika ikiwa ukingo
utaporomoka.
7. Kuwa ukianzisha mwendo wa mbele pole pole na kwa
tahadhari.
8. Tumia uzito au kibebea mzigo kizito kulingana na maelekezo
yaliyokuja na kinasa nyasi. USIENDESHE mashine kwenye
milima zaidi ya digrii 10 (kiwango 18%) ukiwa unatumia
kinasa nyasi.
9. USIWEKE mguu wako chini ukijaribu kudhibiti maishine.
10. USIENDESHE mashine kwenye nyasi zenye unyevu.
Kupungua kwa nguvu ya magurudumu kukamata chini
kunaweza kusababisha iteleze.
11. Chagua mwendo wa pole pole ili usihitajike kusimama au
kubadilisha mwendo kwenye mteremko. Matairi yanaweza
kupoteza nguvu ya kukamata chini kwenye miteremko hata
kama breki zinafanya kazi vizuri.
12. USIENDESHE mashine katika hali yoyote ambapo nguvu
ya magurudumu kukamata chini, uendeshaji au uimara
hauaminiki.
13. Weka mashine ikiwa kwenye gia wakati wote unapoteremka
mteremko. USIWEKE gia huru (au kuwasha uwachiliaji wa
gia kiotomatiki) na kuteremka mteremko bila nishati.
Uandaaji
1. Soma, elewa, na ufuate maelekezo na onyo zilizo katika
mwongozo huu na kwenye mashine, injini na viambatisho.
Jua udhibiti na matumizi bora ya mashine kabla ya kuwasha.
2. Ni watu wazima, wenye kuwajibika pekee wataendesha
mashine na baada ya maelekezo yanayofaa.
3. Data inaonyesha kwamba waendeshaji wenye miaka 60 na
zaidi, wanahusika kwa asilimia kubwa majeraha yanayohusu
mashine ya kukatia nyasi. Waendeshaji hawa wanapaswa
kutathmini uwezo wao wa kuendesha mashine hiyo ya
kukatia nyasi kwa usalama wa kutosha ili kujilinda wao
Usalama wa Mwendeshaji
ONYO
HATARI YA GEZI ZA SUMU. Ekzosi ya injni huwa na monksidi ya
monoksidi ya kaboni, gesi ya sumu inayoweza kukuua ndani ya
dakika chache. HUWEZI kuona, kuinusa, au kuionja. Hata kama
hunusi moshi wa kezosi, bado unaweza kuwa hatarini mwa
gezi ya monoksidi ya kaboni. Ukianza kuhisi ukiwa mojngwa,
kizunguzungu, au kukosa nguvu wakati unatumia kifaa hiki, kizime
na upate hewa safi MARA MOJA. Mtembelee daktari. Huenda ukuwa
umeathiriwa na monoksidi ya kaboni.
• Endesha kifaa hiki nje PEKE YAKE mbali na madirisha, milango na matundu
ili kupunguza hatari ya gesi ya monoksidi ya kaboni kukusanyika na kuenda
maeneo yenye watu.
• Weka ving'ora vya betri vya monoksidi ya kaboni au weka ving'ora vya betri
vya monoksidi ya kaboni kulingana na maelekezo ya mtengenezaji. Ving'ora
vya moshi haviwezi kutambua gesi ya monoksidi ya kaboni.
• USIENDESHE kifaa hiki ndani ya nyumba, garaji, sehemu ya nyumba
iliyo chini ya ardhi, mahali pa kutambaa, vibanda, au maeneo mengine
yaliyofunikwa kiasi hata kama unatumia feni au milango na madirisha
yamefunguliwa kwa uingizaji hewa. Monoksidi ya kaboni inaweza kukusanyika
haraka katika maeneo haya na ibakie kwa saa kadhaa, hata baada ya kifaa
hiki kuzimwa.
• Weka kifaa hiki upande upepo unatoka WAKATI WOTE na ulenge ekzosi
mbali na maeneo yenye watu.
Summary of Contents for 2691382-00
Page 3: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 3 B A 4 A 5 A 6 A B 7 A 8 A B 9 A 10 A B 11 ...
Page 4: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n www snapper com 4 A B 12 A 13 B A 14 A B 15 A B 16 A 17 ...
Page 51: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 29 es ...
Page 73: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 29 fr ...
Page 95: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 29 pt ...
Page 117: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 29 sw ...
Page 121: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n 3 B A 4 A 5 A 6 A B 7 A 8 A B 9 A 10 A B 11 ...
Page 122: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n www snapper com 4 A B 12 A 13 B A 14 A B 15 A B 16 A 17 ...
Page 126: ...N o t f o r R e p r o d u c t i o n A B 41 C A B 42 A D C B 38 A B 39 A B 40 ...